Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER

BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER 👇 Baunsa wa msanii KIZZ DANIEL kutoka nchini Nigeria Kelvin Atobiloye Almaarufu kama KELVIN POWER ameingia katika vitabu vya kumbukumbu baada yakuwa baunsa wa kwanza duniani kuajiri baunsa mwenzake kama mlinzi kwake kutokana na umaarufu wake alioupata gafla baada ya kupostiwa na Kizz Daniel katika mitandao yake alipofanya `Challenge' ya wimbo mpya wa Kizz (My G).Hata hivyo inasemekana pia Kizz Daniel alimuongezea mshahara baunsa wake takribani millioni 2 (N 2million) akisema kwamba ameufanya wimbo wake kuwa maarufu mno!
Machapisho ya hivi karibuni

KAZI ZIPO AJIRA HAKUNA

Tajiri mmoja nchini China Alisema; Weka mbele ya Nyani Ndizi na Pesa, Nyani atachagua ndizi; kwasababu hajui Kwamba Pesa inaweza kununua ndizi nyingi zaidi ya zile ukizoweka mbele yake; Weka vitu viwili Mbele ya Mtu; AJIRA na KAZI; Wengi wetu tunaweza chagua AJIRA sababu kuna Mshahara; Tunapenda vitu visivyotuumiza vichwa Kuna kitu tunasahau KAZI inaweza kukupa PESA Zaidi ya Mshahara Maskini anaendelea kuwa Maskini sababu hajafundishwa namna yakuchungulia  Fursa kwenye Kazi zake Binafsi (UJASIRIAMALI) Huwa tunachukua muda mwingi kusoma shuleni ili tuje tuajiriwe mahali ambapo wote tulio na Ajira tujajua hata Mshahara  haututoshi; tuna madeni kila kona na Stress za kutosha; Faida ya kazi ya mikono yako yaweza kuwa kubwa kuliko Mshahara; Hakikisha unakakitu kako hata kama unaingiza Mia mbili; lakini wewe ndio mmiliki wake; jipe Muda katakuwa tu siku moja... Tutafakari kwa Pamoja Leo Huku tukijikagua nini tufanye; KAZI ZIPO;

JAY Z AMEREJEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII TENA BAADA YA KUFUTA ACCOUNT YAKE YA INSTAGRAM

Jay-Z amerejea kwenye mitandao ya kijamii na kumfanya #Beyonce amfuate ikiwa ni mtu wa kwanza kufanyiwa hivyo, lakini ameendelea na mtindo wake wa kurudi tu wakati ana bidhaa ya kusukuma mitandaoni... wakati huu ni filamu yake mpya. Mwanamuziki huyo maarufu wa muziki wa kufoka ameanzisha upya akaunti yake ya Instagram mapema asubuhi leo na kufichua trela rasmi ujio wa filamu yake ya "Book of Clarence"... akishirikiana na mastaa kama #LaKeithStanfield, #BenedictCumberbatch, #TeyanaTaylor na wengine wengi. Jay-Z aliweka 'post' yake ya kwanza mnamo Novemba 2021 kwenye mtandao huo, akitangaza filamu "The Harder They Fall" ... kisha akapotea kabla ya kurudi leo, ambapo inaelezwa huenda asifute tena akaunti yake. Kionjo cha filamu hiyo kinatoa kiashiria cha ngoma mpya kutoka kwa 'Legend' huyo wa Rap na Hip Hop chini ya mwongozaji #JeymesSamuel ... ambao unaweza kutoka huku ukifuatwa na nyimbo kadhaa kama vile ilivyokuwa kwa wimbo wa '#THTF', au

VITU VITATU PEKEE UNAVYOHITAJI KUSHINDA VIKWAZO KUELEKEA MAFANIKIO

Vitu 3 Pekee Unavohitaji Kushinda Vikwazo Kuelekea Mafanikio Unayoyatafuta. 1. Hisia Imara (Emotional Stability) Kila wakati kuna matukio na watu ambao watakuwa wanafanya mambo ya kukuumiza / kukuhuzunisha ama kukuvunja moyo. Ukiwa mtu ambaye kila KINACHOTOKEA na KILA KINACHOSEMWA kinakuumiza na kufanya usiendelee, Utaishia njiani. Jifunze kuwa IMARA katika HISIA ZAKO na usiruhusu tukio / mtu mmoja akufanye UACHE KABISA kufukuzia NDOTO ZAKO. 2. Kujitafuta Upya (Identinty Re-engineering) Kuna mara kadhaa utadhamiria kufanya jambo fulani lakini baadae MATUKIO ya MAISHA, FURSA, KUJITAMBUA upya n.k kunaweza kukufanya ubadilishe mwelekeo. Kuna watu wamefanikiwa katika biashara ambazo mwanzo hawakuwa wamezifikiria, kuna watu walidhani watazeeka wakifanya Kitu fulani lakini leo wamejikuta wamefanikiwa kwenye Kitu kingine. Kumbuka mipango yako ya leo inategemea unachokiona, usiogope kutumia fursa mpya zinazokuja. Cha muhimu ni kuwa kwa chochote unachofanya: Focus, Consistency na Compete

AJITOLEA KUKUMBATIA WATOTO NJITI WALIOTELEKEZWA KATIKA HOSPITALI

Mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, Mariam Mwakabungu amepokea salamu za pongezi kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kukumbatia watoto njiti waliotelekezwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Amana ili kuwawezesha kukua vizuri. Salamu hizo zimeambatana na na motisha ya shilingi milioni 2 kutoka kwa Rais Samia. Una maoni gani kuhusu wema huu na hatua ya Rais? PICHA: Msaada wa maktaba Kumbuka kutumia lugha ya staha.

TITANIC YA MWAKA 1997 IMEREJESHWA TENA KWENYE MTANDAO

Mtandao maarufu wa kutazama filamu duniani wa Netflix umeeleza kuwa filamu ya Titanic ya mwaka 1997 itarejeshwa tena kwenye mtandao huo, Julai 1 ya mwaka huu wa 2023 kufuatia maombi ya watu wengi juu ya kurejeshwa kwake kutokana na tukio la kuzama kwa Titanic Submarine. Kwa Taarifa zaidi za kiburudani endelea kufatilia MTULYA MEDIA #MTULYA MEDIA updates

MWANZILISHI WA PRECISION AIR TANZANIA

𝙈𝙞𝙘𝙝𝙖𝙚𝙡 𝙉𝙜𝙖𝙡𝙚𝙠𝙪 𝙎𝙝𝙞𝙧𝙞𝙢𝙖 (aliyezaliwa 1943) alikuwa ni Mtanzania mfanyabiashara, mjasiriamali, na mfadhili. Yeye ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa 𝑷𝒓𝒆𝒄𝒊𝒔𝒊𝒐𝒏 𝑨𝒊𝒓, shirika kubwa la ndege linalomilikiwa na watu binafsi nchini Tanzania. Michael Shirima alianzisha Precision Air mnamo mwaka 1993. Ilianza kama kampuni ya kibinafsi ya kukodisha ndege inayoendesha ndege aina ya Piper Aztec yenye viti vitano. Biashara yake ya awali ilihusu kutoa mawasiliano kwa watalii wanaotembelea vivutio vya asili vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kreta ya Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania, Kisiwa cha Zanzibar katika Bahari ya Hindi na maeneo mengine ya nchi kutoka Arusha mjini kama kitovu chake. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za usafiri wa anga wakati nchi ilipoanza uchumi wa soko huria kuliifanya Precision Air kufanya safari zake zilizopangwa na kudumisha Arusha kama kituo chake kikuu. Safari za kwanza za ndege zilipangwa kwa kutumia ndege ya injini moja ya viti saba m