Njia 6 Unazoweza Kutumia Kutengeneza "Passive Income" ___Passive Income ni aina ya kipato ambacho unakipata bila kulazimika kuendelea kufanya kazi. Kulingana na kipato unachokipata sasa na maarifa yako juu ya mambo mbalimbali... ...unaweza kuamua kutumia njia zifuatazo kuzalisha “Passive Income” Yako. 1. Gawio La Faida (Dividend Income) Aina hii ya kipato inatokana na kuwekeza kwenye hisa za makampuni mbalimbali. Katika aina hii ya uwekezaji, ni kuwa unanunua umiliki wa kampuni fulani. Kwa hapa Tanzania, kuna makampuni kadhaa yameorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE), unaweza kununua hisa zake. Mfano: Benki ya CRDB. Baada ya kununua, kila mwisho wa mwaka kampuni inaweza kuamua kugawia wanahisa wake sehemu ya faida iliyopata... ...baada ya kuamuliwa na bodi ya wakurugenzi ya kampuni husika. Ile pesa ambayo unagawiwa, baada ya kampuni kutengeneza faida ndio huitwa “Dividend Income”
UBUNIFU|SANAA|HAMASA ZA KIMAISHA