Aina Za Marafiki Ambao Unawahitaji Kwenye Maisha Yako Ili Utimize Malengo Yako Kwa Kasi. Katika maisha yako kuna aina ya watu ambao unawahitaji... ...ili uweze kufanikiwa katika maisha yako na ili uharakishe kufika kule ambako unataka kufika. Marafiki hawa huwa hawaji kwa bahati bali... ...unatakiwa kuweka mkakati na juhudi maalumu za kuweza kuwapata ili wawe msaada kwako. Leo ningependa tuangalie aina ya marafiki ambao kila aliyefanikiwa aliweka juhudi kuwa nao. Swali kubwa hapa kwako ni je, wewe unao marafiki wa namna hiyo? 1. Rafiki anayeitwa “MUST FRIEND” Huyu ni rafiki ambaye ni wa muhimu sana katika maisha yako... ...na ambaye kila linapotokea jambo kubwa linalohusu maisha yako huwa lazima umtafute ili uongee naye. Rafiki huyu inawezekana usiwe unaonana naye kila siku au mara kwa mara... ...lakini ni mtu ambaye unajua kuwa kwa jambo lolote lile kubwa linalohusu maisha yako ni lazima utamshirikisha. Mara nyingi rafiki wa namna hii unamwamini sana... ...na hauna hofu
UBUNIFU|SANAA|HAMASA ZA KIMAISHA