Ruka hadi kwenye maudhui makuu

AINA ZA MARAFIKI AMBAO UNAWAHITAJI KWENYE MAISHA

Aina Za Marafiki Ambao Unawahitaji Kwenye Maisha Yako Ili Utimize Malengo Yako Kwa Kasi. Katika maisha yako kuna aina ya watu ambao unawahitaji... ...ili uweze  kufanikiwa katika maisha yako na ili uharakishe kufika kule ambako unataka kufika. Marafiki hawa huwa hawaji kwa bahati bali... ...unatakiwa kuweka mkakati na juhudi maalumu za kuweza kuwapata ili wawe msaada kwako. Leo ningependa tuangalie aina ya marafiki ambao kila aliyefanikiwa aliweka juhudi kuwa nao. Swali kubwa hapa kwako ni je, wewe unao marafiki wa namna hiyo? 1. Rafiki anayeitwa “MUST FRIEND” Huyu ni rafiki ambaye ni wa muhimu sana katika maisha yako... ...na ambaye kila linapotokea jambo kubwa linalohusu maisha yako huwa lazima umtafute ili uongee naye. Rafiki huyu inawezekana usiwe unaonana naye kila siku au mara kwa mara... ...lakini ni mtu ambaye unajua kuwa kwa jambo lolote lile kubwa linalohusu maisha yako ni lazima utamshirikisha. Mara nyingi rafiki wa namna hii unamwamini sana... ...na hauna hofu kwamba hata ukimwambia mambo yako ya ndani basi kesho yake hautayasikia yakiwa nje yanazungumzwa. Kila unapokuwa na jambo gumu sana la kuhusu maisha yako na unapata shida na maamuzi ya kuchukua... ...basi rafiki huyu ndiye ambaye utamtafuta na kupata ushauri wake. Mtu wa namna hii ni kwamba shida yako huwa shida yake... ...na unapokuwa umefanikiwa ama kufurahi naye huwa anafurahi pamoja nawe kwa dhati kabisa. Unamuamini kuwa wakati wowote ule utakapohitaji msaada wake... ...basi atajitahidi afanye kila anachoweza kilicho ndani ya uwezo wake ili akusaidie. div class="separator" style="clear: both;">

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER

BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER 👇 Baunsa wa msanii KIZZ DANIEL kutoka nchini Nigeria Kelvin Atobiloye Almaarufu kama KELVIN POWER ameingia katika vitabu vya kumbukumbu baada yakuwa baunsa wa kwanza duniani kuajiri baunsa mwenzake kama mlinzi kwake kutokana na umaarufu wake alioupata gafla baada ya kupostiwa na Kizz Daniel katika mitandao yake alipofanya `Challenge' ya wimbo mpya wa Kizz (My G).Hata hivyo inasemekana pia Kizz Daniel alimuongezea mshahara baunsa wake takribani millioni 2 (N 2million) akisema kwamba ameufanya wimbo wake kuwa maarufu mno!

JAY Z AMEREJEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII TENA BAADA YA KUFUTA ACCOUNT YAKE YA INSTAGRAM

Jay-Z amerejea kwenye mitandao ya kijamii na kumfanya #Beyonce amfuate ikiwa ni mtu wa kwanza kufanyiwa hivyo, lakini ameendelea na mtindo wake wa kurudi tu wakati ana bidhaa ya kusukuma mitandaoni... wakati huu ni filamu yake mpya. Mwanamuziki huyo maarufu wa muziki wa kufoka ameanzisha upya akaunti yake ya Instagram mapema asubuhi leo na kufichua trela rasmi ujio wa filamu yake ya "Book of Clarence"... akishirikiana na mastaa kama #LaKeithStanfield, #BenedictCumberbatch, #TeyanaTaylor na wengine wengi. Jay-Z aliweka 'post' yake ya kwanza mnamo Novemba 2021 kwenye mtandao huo, akitangaza filamu "The Harder They Fall" ... kisha akapotea kabla ya kurudi leo, ambapo inaelezwa huenda asifute tena akaunti yake. Kionjo cha filamu hiyo kinatoa kiashiria cha ngoma mpya kutoka kwa 'Legend' huyo wa Rap na Hip Hop chini ya mwongozaji #JeymesSamuel ... ambao unaweza kutoka huku ukifuatwa na nyimbo kadhaa kama vile ilivyokuwa kwa wimbo wa '#THTF', au

HIVI WEWE UNATAKA KUWA MMOJA WAO??

Hivi na wewe unataka kuwa mmoja wao? Mwanasayansi maarufu, Randy Pausch aliwahi kusema... “Sio yale ambayo TUNAYAFANYA ndio yatatuletea MAJUTO mengi hapo baadaye, bali yale AMBAYO HATUJAYAFANYA ndio TUTAJUTIA ZAIDI”. Watu wengi sana huwa wanaacha kufanya kwa sababu ya kuhofia kupata MATOKEO MABAYA. Yaani, mtu kabla hajaanza kufanya anawaza namna ATAKAVYOFELI... ...kabla hajajaribu anawaza ATAKAVYOKATALIWA n.k Matokeo yake, badala ya kuchukua HATUA, kila siku anabakia KUPANGA na KUSIMULIA anachotaka kukifanya. Usiwe mmoja wa wale ambao WAKISHAZEEKA watakuwa wanajutia na kusema... ...“Yaani, afadhali ningekuwa na UJASIRI wa kufanya wakati ule”. Leo kuna mambo mengi ambayo ingawa UNASINGIZIA kuwa hauna MUDA na FEDHA... ...ukichunguza vizuri Ndani ya MOYO wako ni kwa sababu UNAOGOPA TU. Naomba nikukumbushe kuwa MIAKA inakwenda. Kuna mambo USIPOCHUKUA HATUA na kuanza kuyafanya LEO... ...utatamani kuyafanya HUKO MBELENI na HAITAWEZEKANA, anza Leo.