Tajiri mmoja nchini China Alisema; Weka mbele ya Nyani Ndizi na Pesa, Nyani atachagua ndizi; kwasababu hajui Kwamba Pesa inaweza kununua ndizi nyingi zaidi ya zile ukizoweka mbele yake; Weka vitu viwili Mbele ya Mtu; AJIRA na KAZI; Wengi wetu tunaweza chagua AJIRA sababu kuna Mshahara; Tunapenda vitu visivyotuumiza vichwa Kuna kitu tunasahau KAZI inaweza kukupa PESA Zaidi ya Mshahara Maskini anaendelea kuwa Maskini sababu hajafundishwa namna yakuchungulia Fursa kwenye Kazi zake Binafsi (UJASIRIAMALI) Huwa tunachukua muda mwingi kusoma shuleni ili tuje tuajiriwe mahali ambapo wote tulio na Ajira tujajua hata Mshahara haututoshi; tuna madeni kila kona na Stress za kutosha; Faida ya kazi ya mikono yako yaweza kuwa kubwa kuliko Mshahara; Hakikisha unakakitu kako hata kama unaingiza Mia mbili; lakini wewe ndio mmiliki wake; jipe Muda katakuwa tu siku moja... Tutafakari kwa Pamoja Leo Huku tukijikagua nini tufanye; KAZI ZIPO;
UBUNIFU|SANAA|HAMASA ZA KIMAISHA