Ruka hadi kwenye maudhui makuu

VITU VITATU PEKEE UNAVYOHITAJI KUSHINDA VIKWAZO KUELEKEA MAFANIKIO

Vitu 3 Pekee Unavohitaji Kushinda Vikwazo Kuelekea Mafanikio Unayoyatafuta. 1. Hisia Imara (Emotional Stability) Kila wakati kuna matukio na watu ambao watakuwa wanafanya mambo ya kukuumiza / kukuhuzunisha ama kukuvunja moyo. Ukiwa mtu ambaye kila KINACHOTOKEA na KILA KINACHOSEMWA kinakuumiza na kufanya usiendelee, Utaishia njiani. Jifunze kuwa IMARA katika HISIA ZAKO na usiruhusu tukio / mtu mmoja akufanye UACHE KABISA kufukuzia NDOTO ZAKO. 2. Kujitafuta Upya (Identinty Re-engineering) Kuna mara kadhaa utadhamiria kufanya jambo fulani lakini baadae MATUKIO ya MAISHA, FURSA, KUJITAMBUA upya n.k kunaweza kukufanya ubadilishe mwelekeo. Kuna watu wamefanikiwa katika biashara ambazo mwanzo hawakuwa wamezifikiria, kuna watu walidhani watazeeka wakifanya Kitu fulani lakini leo wamejikuta wamefanikiwa kwenye Kitu kingine. Kumbuka mipango yako ya leo inategemea unachokiona, usiogope kutumia fursa mpya zinazokuja. Cha muhimu ni kuwa kwa chochote unachofanya: Focus, Consistency na Competency. (Usiyumbishwe, Uwe na Mwendelezo na Jenga Uwezo) 3. Kufanya, Kufanya, Kufanya. (Be on the Move) Kuna wakati hautajisikia kufanya, wewe amua KUFANYA. Kuna wakati kila dalili itaonyesha hausogei hatua, wewe fanya. Moja ya MAAMUZI unatakiwa kuyafanya MAISHA YAKO yote ni kuwa UTAENDELEA KUFANYA kila siku bila kujali vizuizi. USIPIME siku yako kwa MATOKEO peke yake, IPIME pia kwa MBEGU UNAZOPANDA ambazo kesho zitatoa MATUNDA. Usikubali siku ipite haujafanya Kitu hata kama ni kidogo sana. Nakutakia mafanikio mema.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER

BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER 👇 Baunsa wa msanii KIZZ DANIEL kutoka nchini Nigeria Kelvin Atobiloye Almaarufu kama KELVIN POWER ameingia katika vitabu vya kumbukumbu baada yakuwa baunsa wa kwanza duniani kuajiri baunsa mwenzake kama mlinzi kwake kutokana na umaarufu wake alioupata gafla baada ya kupostiwa na Kizz Daniel katika mitandao yake alipofanya `Challenge' ya wimbo mpya wa Kizz (My G).Hata hivyo inasemekana pia Kizz Daniel alimuongezea mshahara baunsa wake takribani millioni 2 (N 2million) akisema kwamba ameufanya wimbo wake kuwa maarufu mno!

JAY Z AMEREJEA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII TENA BAADA YA KUFUTA ACCOUNT YAKE YA INSTAGRAM

Jay-Z amerejea kwenye mitandao ya kijamii na kumfanya #Beyonce amfuate ikiwa ni mtu wa kwanza kufanyiwa hivyo, lakini ameendelea na mtindo wake wa kurudi tu wakati ana bidhaa ya kusukuma mitandaoni... wakati huu ni filamu yake mpya. Mwanamuziki huyo maarufu wa muziki wa kufoka ameanzisha upya akaunti yake ya Instagram mapema asubuhi leo na kufichua trela rasmi ujio wa filamu yake ya "Book of Clarence"... akishirikiana na mastaa kama #LaKeithStanfield, #BenedictCumberbatch, #TeyanaTaylor na wengine wengi. Jay-Z aliweka 'post' yake ya kwanza mnamo Novemba 2021 kwenye mtandao huo, akitangaza filamu "The Harder They Fall" ... kisha akapotea kabla ya kurudi leo, ambapo inaelezwa huenda asifute tena akaunti yake. Kionjo cha filamu hiyo kinatoa kiashiria cha ngoma mpya kutoka kwa 'Legend' huyo wa Rap na Hip Hop chini ya mwongozaji #JeymesSamuel ... ambao unaweza kutoka huku ukifuatwa na nyimbo kadhaa kama vile ilivyokuwa kwa wimbo wa '#THTF', au

HIVI WEWE UNATAKA KUWA MMOJA WAO??

Hivi na wewe unataka kuwa mmoja wao? Mwanasayansi maarufu, Randy Pausch aliwahi kusema... “Sio yale ambayo TUNAYAFANYA ndio yatatuletea MAJUTO mengi hapo baadaye, bali yale AMBAYO HATUJAYAFANYA ndio TUTAJUTIA ZAIDI”. Watu wengi sana huwa wanaacha kufanya kwa sababu ya kuhofia kupata MATOKEO MABAYA. Yaani, mtu kabla hajaanza kufanya anawaza namna ATAKAVYOFELI... ...kabla hajajaribu anawaza ATAKAVYOKATALIWA n.k Matokeo yake, badala ya kuchukua HATUA, kila siku anabakia KUPANGA na KUSIMULIA anachotaka kukifanya. Usiwe mmoja wa wale ambao WAKISHAZEEKA watakuwa wanajutia na kusema... ...“Yaani, afadhali ningekuwa na UJASIRI wa kufanya wakati ule”. Leo kuna mambo mengi ambayo ingawa UNASINGIZIA kuwa hauna MUDA na FEDHA... ...ukichunguza vizuri Ndani ya MOYO wako ni kwa sababu UNAOGOPA TU. Naomba nikukumbushe kuwa MIAKA inakwenda. Kuna mambo USIPOCHUKUA HATUA na kuanza kuyafanya LEO... ...utatamani kuyafanya HUKO MBELENI na HAITAWEZEKANA, anza Leo.