Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 24, 2022

MTOTO WA SIMBACHAWENE AMEHUKUMIWA KULIPA FAINI

Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya. Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu. Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima. Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita

SIMBA QUEENS YATINGA FAINAL KWA USHINDI WA 5.1

Klabu ya Simba Queens imeibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya klabu ya Wanawake ya AS Kigali ya Rwanda katika nusu fainali ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ukanda wa CECAFA. Simba Queens imetinga fainali na itachuana na timu ya She Corporate ya Uganda iliyotinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Commercial Bank FC ya Ethiopia. Mchezo wa fainali utachezwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi mnamo Agosti 27.

BAILLY AMWAGA WINO MARSEILLE

📝 𝐃𝐎𝐍𝐄 𝐃𝐄𝐀𝐋: Klabu ya Olympique Marseille imekamilisha usajili wa mlinzi wa Manchester United, Eric Bailly (28) kwa mkataba wa mkopo wenye chaguo la kumchukua jumla.