Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya.
Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu.
Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima.
Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita.
BAUNSA WA KWANZA DUNIANI KUAJIRI BAUNSA WAKE PIA~KELVIN POWER 👇 Baunsa wa msanii KIZZ DANIEL kutoka nchini Nigeria Kelvin Atobiloye Almaarufu kama KELVIN POWER ameingia katika vitabu vya kumbukumbu baada yakuwa baunsa wa kwanza duniani kuajiri baunsa mwenzake kama mlinzi kwake kutokana na umaarufu wake alioupata gafla baada ya kupostiwa na Kizz Daniel katika mitandao yake alipofanya `Challenge' ya wimbo mpya wa Kizz (My G).Hata hivyo inasemekana pia Kizz Daniel alimuongezea mshahara baunsa wake takribani millioni 2 (N 2million) akisema kwamba ameufanya wimbo wake kuwa maarufu mno!
Maoni
Chapisha Maoni