Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya TANZIA

TITANIC YA MWAKA 1997 IMEREJESHWA TENA KWENYE MTANDAO

Mtandao maarufu wa kutazama filamu duniani wa Netflix umeeleza kuwa filamu ya Titanic ya mwaka 1997 itarejeshwa tena kwenye mtandao huo, Julai 1 ya mwaka huu wa 2023 kufuatia maombi ya watu wengi juu ya kurejeshwa kwake kutokana na tukio la kuzama kwa Titanic Submarine. Kwa Taarifa zaidi za kiburudani endelea kufatilia MTULYA MEDIA #MTULYA MEDIA updates

MWANZILISHI WA PRECISION AIR TANZANIA

𝙈𝙞𝙘𝙝𝙖𝙚𝙡 𝙉𝙜𝙖𝙡𝙚𝙠𝙪 𝙎𝙝𝙞𝙧𝙞𝙢𝙖 (aliyezaliwa 1943) alikuwa ni Mtanzania mfanyabiashara, mjasiriamali, na mfadhili. Yeye ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa 𝑷𝒓𝒆𝒄𝒊𝒔𝒊𝒐𝒏 𝑨𝒊𝒓, shirika kubwa la ndege linalomilikiwa na watu binafsi nchini Tanzania. Michael Shirima alianzisha Precision Air mnamo mwaka 1993. Ilianza kama kampuni ya kibinafsi ya kukodisha ndege inayoendesha ndege aina ya Piper Aztec yenye viti vitano. Biashara yake ya awali ilihusu kutoa mawasiliano kwa watalii wanaotembelea vivutio vya asili vya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kreta ya Ngorongoro, kaskazini mwa Tanzania, Kisiwa cha Zanzibar katika Bahari ya Hindi na maeneo mengine ya nchi kutoka Arusha mjini kama kitovu chake. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma za usafiri wa anga wakati nchi ilipoanza uchumi wa soko huria kuliifanya Precision Air kufanya safari zake zilizopangwa na kudumisha Arusha kama kituo chake kikuu. Safari za kwanza za ndege zilipangwa kwa kutumia ndege ya injini moja ya viti saba m

MAMA KASEMA

MTOTO WA SIMBACHAWENE AMEHUKUMIWA KULIPA FAINI

Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya. Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu. Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima. Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita