Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

AINA ZA MARAFIKI AMBAO UNAWAHITAJI KWENYE MAISHA

Aina Za Marafiki Ambao Unawahitaji Kwenye Maisha Yako Ili Utimize Malengo Yako Kwa Kasi. Katika maisha yako kuna aina ya watu ambao unawahitaji... ...ili uweze  kufanikiwa katika maisha yako na ili uharakishe kufika kule ambako unataka kufika. Marafiki hawa huwa hawaji kwa bahati bali... ...unatakiwa kuweka mkakati na juhudi maalumu za kuweza kuwapata ili wawe msaada kwako. Leo ningependa tuangalie aina ya marafiki ambao kila aliyefanikiwa aliweka juhudi kuwa nao. Swali kubwa hapa kwako ni je, wewe unao marafiki wa namna hiyo? 1. Rafiki anayeitwa “MUST FRIEND” Huyu ni rafiki ambaye ni wa muhimu sana katika maisha yako... ...na ambaye kila linapotokea jambo kubwa linalohusu maisha yako huwa lazima umtafute ili uongee naye. Rafiki huyu inawezekana usiwe unaonana naye kila siku au mara kwa mara... ...lakini ni mtu ambaye unajua kuwa kwa jambo lolote lile kubwa linalohusu maisha yako ni lazima utamshirikisha. Mara nyingi rafiki wa namna hii unamwamini sana... ...na hauna hofu

MIGOGORO KWENYE NDOA KUHUSU PESA

Maeneo Yanayoleta Migogoro Kwenye Ndoa Kuhusu Pesa. ____1. Mikopo ya Kificho Umeshawahi kuwa na mwenzi wako halafu unakuja kupata taarifa... ...kuwa anadaiwa sana na mnatakiwa ku lipa? Mbaya zaidi, taarifa hakukupatia wewe mwenyewe... ...umeipata kwa njia nyingine. Wanandoa wengi sana wameingia kwenye changamoto za kifedha... ...kwa sababu ya mmoja wao kuingia kwenye mikopo bila taarifa ya mwingine. Na kwenye kulipa inahitaji uwajibikaji wa wote. Wakati mwingine unakuta mtu hadi kachukua “DOCUMENT” fulani... ...kimya kimya na kaipeleka (Kadi ya gari, hati ya nyumba etc). Mwingine anapokuja kugundua huwa inaweza... ...kupelekea migogoro mikubwa sana katika mahusiano ya ndoa. Ni muhimu sana kujitahidi KUEPUKA mikopo ya kificho ili kuendeleza amani ya ndoa yenu.

HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAMA KASEMA

VITAMBO VYA MAAFISA HABARI

“Leo niliwapigia simu maafisa Habari wote wa Ligi Kuu kuwaeleza maelekezo ya CAF kuhusu nusu fainali, Media Officer unatakiwa uwe vipi….. “Simu ya Ahmed Ally iliita haikupokelewa, bahati nzuri nilipiga tena akapokea nikasikia upepo tu, nikaumuulza vipi akaniambia anaenda Mtwara. “Nikamuuliza kuna nini akasema anaenda kucheza nusu fainali, nikamwambia nusu fainali nchi Hii ni moja tu, sasa kama CAF wanampgia afisa habari alafu kuna upepo namna ile unakuwa disqualified,” Ally Kamwe

MPINZANI WA YANGA KWENYE CAF

Marumo Gallants wanacheza mpira wa kasi sana, mshambuliaji wao hatari ni Ranga Chivaviro ambaye ana mabao 5 sawa na Mayele, yaani utengenezaji wao wa magoli ni mkubwa hivyo Yanga wanatakiwa kuwa makini. Wana nidhamu ya kutopoteza mchezo pia, hawaruhusu kirahisi magoli"- "Tangu 2019 hawa Marumo Gallants katika michezo ya Kimataifa hawajapoteza mchezo katika uwanja wa nyumbani, kila mchezo wamefunga bao". Sifa yao kubwa ni kwenye mchezo wa kasi" - #Yanga #MarumoGallants #MTULYAMEDIA

MTOTO WA SIMBACHAWENE AMEHUKUMIWA KULIPA FAINI

Mfanyabiashara, James Simbachawene (24) ambaye ni mtoto wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amehukumiwa kulipa faini ya Sh250, 000 na kufungiwa leseni yake ya udereva kwa miezi sita baada ya kukiri makosa matatu. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani leo Jumatano Agosti 24, 2022 jioni na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali, Daisy Makakala, mbele ya Hakimu Mkazi Aron Lyamuya. Mashitaka hayo ni pamoja na kuendesha gari kwa hatari, kuendesha gari akiwa amelewa na kuendesha gari bila kuwa na bima. Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Simbachawene alikiri na ndipo hakimu Lyamuya alipoahirisha kesi ili kumwandikia hukumu. Baada ya muda mfupi, ndipo hakimu Lyamuya alimhukumu Simbachawene kulipa faini ya Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari kwa hatari, Sh100,000 kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na Sh50,000 kwa kosa la kuendesha gari bila kuwa na bima. Pamoja na faini hiyo, leseni ya Simbachawene imefungiwa kwa miezi sita