Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

NJIA 6 UNAZOWEZA KUTUMIA KUTENGENEZA PASSIVE INCOME

Njia 6 Unazoweza Kutumia Kutengeneza "Passive Income" ___Passive Income ni aina ya kipato ambacho unakipata bila kulazimika kuendelea kufanya kazi. Kulingana na kipato unachokipata sasa na maarifa yako juu ya mambo mbalimbali... ...unaweza kuamua kutumia njia zifuatazo kuzalisha “Passive Income” Yako. 1. Gawio La Faida (Dividend Income) Aina hii ya kipato inatokana na kuwekeza kwenye hisa za makampuni mbalimbali. Katika aina hii ya uwekezaji, ni kuwa unanunua umiliki wa kampuni fulani. Kwa hapa Tanzania, kuna makampuni kadhaa yameorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE), unaweza kununua hisa zake. Mfano: Benki ya CRDB. Baada ya kununua, kila mwisho wa mwaka kampuni inaweza kuamua kugawia wanahisa wake sehemu ya faida iliyopata... ...baada ya kuamuliwa na bodi ya wakurugenzi ya kampuni husika. Ile pesa ambayo unagawiwa, baada ya kampuni kutengeneza faida ndio huitwa “Dividend Income”

HIVI WEWE UNATAKA KUWA MMOJA WAO??

Hivi na wewe unataka kuwa mmoja wao? Mwanasayansi maarufu, Randy Pausch aliwahi kusema... “Sio yale ambayo TUNAYAFANYA ndio yatatuletea MAJUTO mengi hapo baadaye, bali yale AMBAYO HATUJAYAFANYA ndio TUTAJUTIA ZAIDI”. Watu wengi sana huwa wanaacha kufanya kwa sababu ya kuhofia kupata MATOKEO MABAYA. Yaani, mtu kabla hajaanza kufanya anawaza namna ATAKAVYOFELI... ...kabla hajajaribu anawaza ATAKAVYOKATALIWA n.k Matokeo yake, badala ya kuchukua HATUA, kila siku anabakia KUPANGA na KUSIMULIA anachotaka kukifanya. Usiwe mmoja wa wale ambao WAKISHAZEEKA watakuwa wanajutia na kusema... ...“Yaani, afadhali ningekuwa na UJASIRI wa kufanya wakati ule”. Leo kuna mambo mengi ambayo ingawa UNASINGIZIA kuwa hauna MUDA na FEDHA... ...ukichunguza vizuri Ndani ya MOYO wako ni kwa sababu UNAOGOPA TU. Naomba nikukumbushe kuwa MIAKA inakwenda. Kuna mambo USIPOCHUKUA HATUA na kuanza kuyafanya LEO... ...utatamani kuyafanya HUKO MBELENI na HAITAWEZEKANA, anza Leo.

DALILI 6 ZITAKAZOKUONYESHA KUWA HALI YAKO YA KIFEDHA IKO KWENYE HATARI

Dalili 6 Zitakazokuonesha Kuwa Hali Yako Ya Kifedha Iko Kwenye Hatari. ____Dalili Ya Kwanza: Unakopa Mara Kwa Mara Kwa Mahitaji Ya Msingi. Ni kawaida kabisa kwa mwanadamu kupata changamoto za kifedha... ...ila ukiona changamoto zako zinajirudia rudia kila wakati, ujue kuna tatizo. Ukiona kila wakati unakopa kwa ajili ya mahitaji ya msingi kama vile: Una madeni mengi ya chakula dukani... Unadaiwa sana mavazi (nguo, viatu n.k)... Kila ikifika wakati wa kulipa kodi lazima ukope... ...kila wakati wa kupeleka shule lazima ukope ada ya watoto n.k Hapa sizungumzii jambo ambalo huwa linatokea mara moja moja tu... ...bali lile ambalo huwa linatokea mara kwa mara. @joelnanauka

AINA ZA MARAFIKI AMBAO UNAWAHITAJI KWENYE MAISHA

Aina Za Marafiki Ambao Unawahitaji Kwenye Maisha Yako Ili Utimize Malengo Yako Kwa Kasi. Katika maisha yako kuna aina ya watu ambao unawahitaji... ...ili uweze  kufanikiwa katika maisha yako na ili uharakishe kufika kule ambako unataka kufika. Marafiki hawa huwa hawaji kwa bahati bali... ...unatakiwa kuweka mkakati na juhudi maalumu za kuweza kuwapata ili wawe msaada kwako. Leo ningependa tuangalie aina ya marafiki ambao kila aliyefanikiwa aliweka juhudi kuwa nao. Swali kubwa hapa kwako ni je, wewe unao marafiki wa namna hiyo? 1. Rafiki anayeitwa “MUST FRIEND” Huyu ni rafiki ambaye ni wa muhimu sana katika maisha yako... ...na ambaye kila linapotokea jambo kubwa linalohusu maisha yako huwa lazima umtafute ili uongee naye. Rafiki huyu inawezekana usiwe unaonana naye kila siku au mara kwa mara... ...lakini ni mtu ambaye unajua kuwa kwa jambo lolote lile kubwa linalohusu maisha yako ni lazima utamshirikisha. Mara nyingi rafiki wa namna hii unamwamini sana... ...na hauna hofu

MIGOGORO KWENYE NDOA KUHUSU PESA

Maeneo Yanayoleta Migogoro Kwenye Ndoa Kuhusu Pesa. ____1. Mikopo ya Kificho Umeshawahi kuwa na mwenzi wako halafu unakuja kupata taarifa... ...kuwa anadaiwa sana na mnatakiwa ku lipa? Mbaya zaidi, taarifa hakukupatia wewe mwenyewe... ...umeipata kwa njia nyingine. Wanandoa wengi sana wameingia kwenye changamoto za kifedha... ...kwa sababu ya mmoja wao kuingia kwenye mikopo bila taarifa ya mwingine. Na kwenye kulipa inahitaji uwajibikaji wa wote. Wakati mwingine unakuta mtu hadi kachukua “DOCUMENT” fulani... ...kimya kimya na kaipeleka (Kadi ya gari, hati ya nyumba etc). Mwingine anapokuja kugundua huwa inaweza... ...kupelekea migogoro mikubwa sana katika mahusiano ya ndoa. Ni muhimu sana kujitahidi KUEPUKA mikopo ya kificho ili kuendeleza amani ya ndoa yenu.

HABARI KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAMA KASEMA